Saturday, October 29, 2011

Friday, October 28, 2011

WAO NA SISI!!!

ZITO APELEKWA INDIA CHINI YA UANGALIZI MKALI
Kuna kitu kinaniuma sana moyoni mwangu, huwa naumia sana pale ninapopona viongozi wetu wanajifikiria wao tu, na sisi kutuona kama si watu bali ni wadudu.
Hivi juzi juzi tulisika Mwakyembe kapelekwa india kutibiwa, kila chombo cha habari kiliripoti kuhusu hilo.  Hilo ni sawa kwani kutibiwa si kosa na wala mtu hakuhukumu kwa kutafuta matibabu.

Ila kilichonichoma zaidi ni kwamba  kuna taarifa kwamba mbunge wa kigoma kaskazini Bw. Zito Kabwe nae kapelekwa India kutibiwa baada ya kukutwa na malaria 150,! Jamani mimi hainiingii akilini hata kidogo, malaria tu hii ambayo hata hapa Tanzania ina uwezo wa kutibiwa eti mtu anapelekwa India.  Sisi mbona kila siku tunaumwa na kufa kila siku na hiyo malaria!!! mbona hakuna hata mmoja aliyepelekwa India hata hapo kenya kutibiwa.!

Hii ni changamoto kwenu wakubwa wetu, hivi ni kweli tunashindwa kuzalisha madaktari bingwa ili hata sisi tusiokuwa na uwezo wa kwenda india tukafaidika nao!!!???

                                                 NI MTAZAMO TU JAMANI!!!

Monday, October 24, 2011

MTAZAMO WANGU JUU YA KIFO CHA GADAFI

Najua kuna baadhi ya viongozi wa dunia wanafurahia, na wale wapumbavu wa mawazo ambao wanapenda kuwa watumwa wa akili, wale wanaoshikiwa akili na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiendesha maisha yao.Lakini mimi kifo cha Gaddafi kimeniumiza na kinanitia uchungu, kwa sababu ule wakati wa kutawaliwa akili sasa ndio utashamiri.

Alikuwa kiongozi  aliyeona mbali, kitendo cha Gaddafi kutoruhusu nchi yake iingiliwe kiuchumi na super powers Nations, kiliwakera sana, ndio maana wakatafuta kila sababu ya kumtoa hata kwa mtutu ili wao wapate fursa za kuingia pale na kwa asilimia kubwa wameshafanikiwa sasa.

Sasa kaeni musikilize kama waliomuua watapelekwa ICC, na kuhusu nato je!!!??? wale mamilioni wa ndugu zetu waliowauwa wakati wanamtoa Gaddafi, watachukuliwa hatua gani na hao wanaojiita Supper Powers.

NI MTAZAMO TU JAMANI!!!!!!!!!!!!

Wednesday, October 19, 2011

LINDI WATAKA UHURU WA KUUZA KOROSHO

Wakulima wa korosho mkoani lindi, wameitaka serikali iwape uhuru wa kuuza zao hilo kwa watu wanaowafahamu bila ya kujiunga na chama kikuu cha ushirika cha ilulu, walichodai kinawanyonya kimapato.

wakulima hao wamedai kuwa, chama hicho cha ushirika kimeshindwa kuwashirikisha katika shughuli za uuzaji wa zao hilo, ikiwemo upigaji mnada wa korosho, jambo linalowafanya kuamini wanadhulumiwa.

wakizungumza kwa nyakati tofauti mkoani humo, mmoja wa wakulima hao bw.mshingi matandu, ambaye ni mwenyekiti wa chama cha msingi njinjo wilayani kilwa, amesema kuwa, ni muhimu serikali kuingilia kati suala hilo na kuwapa uhuru wa kutafuta soko wenyewe, ili waweze kuuza korosho zao kwa bei wanayoitaka.

kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha msingi cha limalyao kusini, hassan wajihi amesema, chama hicho kimekuwa kikiwatoza kodi kubwa, jambo linaoonesha kuwa, fedha hizo zinatumika kinyume na taratibu.

Tuesday, October 18, 2011

MURJI AMSHINDA ULEDI, MAHAKAMA YATUPILIA MBALI SHAURI LA ULEDI!

                  mbunge wa jimbo la Mtwara mjini akiteta na Mh. Nape Nauye alipotembelea Mtwara





Mahakama ya mkoa Mtwara, imetupilia mbali shauri la aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la mtwar a mjini kwa tiketi ya CUF Bw. Uledi Hassan Abdalah, la kukituhumu chama cha mapinduzi(CCM) kuwa kimechakachua kura za uchaguzi wa ubunge uliofanyika mwaka jana na kumpa ushindi mbunge wa jimbo hilo Bw. Asnen Murji.

Jaji wa mahakama hiyo mh. Selemani Saidi,  ametua uamuzi huo leo kwa madai kuwa upande wa mashtaka haukuwa na ushahidi wa kutosha hususan nyaraka.

MISS MTWARA 2011 AFARIKI DUNIA!

Mnyange aliyechukua taji la miss mtwara 2011 Rahma swai, amefariki dunia usiku wa jana kuamkia leo katika hospitali ya mkoa ligula kutokana na maradhi ya tumbo.

mrembo huyo ambae nyota ya ke ndio kwanza ilikuwa inaanza kung'aa, alifikishwa hospitalini hapo baada ya kulazwa katika zahanati ya sajora, baada ya kuona hali yake inazidi kuwa mbaya, alikimbizwa hospitali ya mkoa wa mtwara ligula ndipo ilipomfika umauti. 

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehem mahali anapostahili, jina la Bwana lihimidiwe, leo na hata milele.  Amina.

Monday, October 17, 2011

Diamond akabidhi msaada hospitali ya ligula mtwara

                              
MSANII anayetamba katika muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava), Naseeb Abdul ‘Diamond’,  ametoa misaada mbalimbali yenye thamani ya sh. 3,500,000 na laki tano katika wodi ya wazazi ya  Hospitali ya Ligula Mkoa Mtwara.



Akikabidhi msaada huo, Diamond alisema  yeye kama msanii amevutiwa kutoa msaada katika wodi ya wazazi kwa kuwa watoto wanaozaliwa watakuwa mashabiki wake na watapenda kazi zake hapo baadaye.  Msaada msaada huo umefadhiliwa na Safari Radio Foundation.

Friday, October 14, 2011

kifo cha nyerere

kifo chake kimetoa mianya kwa viongozi wa tanzania kuitumia nchi kwa manufaa yao na si kama ambavyo yeye alikuwa anaifanyia Tanzania. naumizwa na kuondoka kwake, angekuwapo labda yasingetokea yanayojiri tanzania kwa sasa, uchu wa madaraka unaiua Tanzania yake, yako na yangu.