Wednesday, October 19, 2011

LINDI WATAKA UHURU WA KUUZA KOROSHO

Wakulima wa korosho mkoani lindi, wameitaka serikali iwape uhuru wa kuuza zao hilo kwa watu wanaowafahamu bila ya kujiunga na chama kikuu cha ushirika cha ilulu, walichodai kinawanyonya kimapato.

wakulima hao wamedai kuwa, chama hicho cha ushirika kimeshindwa kuwashirikisha katika shughuli za uuzaji wa zao hilo, ikiwemo upigaji mnada wa korosho, jambo linalowafanya kuamini wanadhulumiwa.

wakizungumza kwa nyakati tofauti mkoani humo, mmoja wa wakulima hao bw.mshingi matandu, ambaye ni mwenyekiti wa chama cha msingi njinjo wilayani kilwa, amesema kuwa, ni muhimu serikali kuingilia kati suala hilo na kuwapa uhuru wa kutafuta soko wenyewe, ili waweze kuuza korosho zao kwa bei wanayoitaka.

kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha msingi cha limalyao kusini, hassan wajihi amesema, chama hicho kimekuwa kikiwatoza kodi kubwa, jambo linaoonesha kuwa, fedha hizo zinatumika kinyume na taratibu.