Friday, June 22, 2012



Lady Jaydee: Ukiniona kwenye harusi usifikirie niko pale kuimba


Mwanamuziki mkongwe na mwenye mafanikio zaidi nchini Tanzania Judith Wambura aka Lady Jaydee amefunguka na kusema kile kinachomkera sana akihudhuria kwenye harusi.

Kupitia mtandao wa Twitter jana komando huyo wa muziki kama anavyojiita amesema watu humpanda kichwani pale wanapodhani popote alipo yupo kwa ajili ya kuimba tu.

“Siwaelewagi watu wanaokuona tu harusini kama mualikwa halafu wanaanza kukung'ang'aniza uimbe wakati hauko kwenye ratiba. Heshimu kazi ya mtu,” aliandika.

Aliongeza, “Halafu wanajua kushupalia hao, utasikia kidogo tu si wimbo mmoja tu, utadhani huo wimbo mtu uliurecord bure studio.”

No comments:

Post a Comment