ZITO APELEKWA INDIA CHINI YA UANGALIZI MKALI
Kuna kitu kinaniuma sana moyoni mwangu, huwa naumia sana pale ninapopona viongozi wetu wanajifikiria wao tu, na sisi kutuona kama si watu bali ni wadudu.Hivi juzi juzi tulisika Mwakyembe kapelekwa india kutibiwa, kila chombo cha habari kiliripoti kuhusu hilo. Hilo ni sawa kwani kutibiwa si kosa na wala mtu hakuhukumu kwa kutafuta matibabu.
Ila kilichonichoma zaidi ni kwamba kuna taarifa kwamba mbunge wa kigoma kaskazini Bw. Zito Kabwe nae kapelekwa India kutibiwa baada ya kukutwa na malaria 150,! Jamani mimi hainiingii akilini hata kidogo, malaria tu hii ambayo hata hapa Tanzania ina uwezo wa kutibiwa eti mtu anapelekwa India. Sisi mbona kila siku tunaumwa na kufa kila siku na hiyo malaria!!! mbona hakuna hata mmoja aliyepelekwa India hata hapo kenya kutibiwa.!
Hii ni changamoto kwenu wakubwa wetu, hivi ni kweli tunashindwa kuzalisha madaktari bingwa ili hata sisi tusiokuwa na uwezo wa kwenda india tukafaidika nao!!!???
NI MTAZAMO TU JAMANI!!!
No comments:
Post a Comment