Friday, June 22, 2012Lady Jaydee: Ukiniona kwenye harusi usifikirie niko pale kuimba


Mwanamuziki mkongwe na mwenye mafanikio zaidi nchini Tanzania Judith Wambura aka Lady Jaydee amefunguka na kusema kile kinachomkera sana akihudhuria kwenye harusi.

Kupitia mtandao wa Twitter jana komando huyo wa muziki kama anavyojiita amesema watu humpanda kichwani pale wanapodhani popote alipo yupo kwa ajili ya kuimba tu.

“Siwaelewagi watu wanaokuona tu harusini kama mualikwa halafu wanaanza kukung'ang'aniza uimbe wakati hauko kwenye ratiba. Heshimu kazi ya mtu,” aliandika.

Aliongeza, “Halafu wanajua kushupalia hao, utasikia kidogo tu si wimbo mmoja tu, utadhani huo wimbo mtu uliurecord bure studio.”

Akon alipuuzia kumsainisha Drake kabla hajaenda YMCMB
Akon kwa hakika ana pua inayonusa vipaji, muulize tu T-Pain na Lady GagaLakini hata hivyo pamoja na kuwa hivyo kuna wakati huwa anashindwa pia kubaini madini na juzi kupitia kipindi "RapFix Live" rapper Kardinal Offishall aliweka wazi kosa alilolifanya

Nilimwambia kuhusu Drake mapema. Nilimwambia, Akon huyu dogo ni staa kwenye TV ni mkali balaa,” alisema Kardinall
Kardinal Offishall alikiona kipaji na uwezo wa Drake kabla ya YMCMB.


Kardinal, kama Drizzy, Anatokea Toronto, lakini alifanikiwa kutoka kabla ya Drake hajafahamika mwaka 2009 na mixtape yake So Far Gone
Nilikutana naye kabla hajaanza kufanya mixtape yake ya kwanza,” alisema. Kitu ambacho nakumbuka kuhusu Drake ni kama alikuwa na njaa ya kutoka kwenye uigizaji kwenda kwenye kurapBaada ya kutoka nilienda na kumwambia Akon, “Nilikuambia”. Lakini hayo ni miongoni mwa mambo ambayo yamefanya kazi kwa Drake na YMCMB. Ana kambi nzuri

Unahisi Drake angekuwa hapo alipo kama Akon angemchukua

Thursday, April 12, 2012

SABABU ZA KIFO CHA KANUMBA ZATAJWA........!!!!

MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.

Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.
“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”
“Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”
Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Alisema sehemu ya maini na majimaji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.KESHO NDANI YA LIFE STYLE!!!!

DARASA LA MAISHA TUTAONGELEA JUU YA KUKUBALI TATIZO NA KULIKABILI.

tutaangalia njia mbalimbali za kukusaidia unapopatwa na matatizo.
Mara nyingi mtu anapopatwa na matatizo hubabaika na kujikuta hana msaada wowote.

 Usikose kusikiliza kesho saa 09:00 asubuhi ndani ya life style!

Wednesday, April 11, 2012

KESHO NDANI YA LIFE STYLE YA 90.5 BEST FM RADIO, TUTADISCUSS NA WEWE KUHUSU TALAKA KAMA NI SULUHU YA MIGOGORO KAYIKA NDOA!! KEEP IN TOUCH!

Nitakuwepo mwenyewe kulisongesha mwanzo mwisho ndani ya studio za 90.5, One & Only super duper presenter Mj wa ukwen'eee!!!

LIPI NI ZITO ZAIDI KATI YA HAYA!!?? KIFO CHA MSANII STEVIN KANUMBA NA JENERALI MWITA KYARO!!??

Watanzania tumeoneshwa kuguswa kwetu na kifo cha msanii nguli wa filamu Tanzania Stevin Kanumba, na kusahau kifo cha mtu muhimu sana kwa Taifa hili Jenerali mwita Kyaro, na kuact kama hana umuhimu kuliko huyu mtu!!! but kumbuka HUU NI MTAZAMO TU!!!

LONG TIME KITAMBO!! I'M COMMING BACK GUYS!


Wapendwa, nilikuwa kimya sana kutokana na majukumu, but narudi very soon!!!! kwa nguvu zote!! just keep in touch with me!!! Thanx!