Friday, June 22, 2012


Akon alipuuzia kumsainisha Drake kabla hajaenda YMCMB




Akon kwa hakika ana pua inayonusa vipaji, muulize tu T-Pain na Lady GagaLakini hata hivyo pamoja na kuwa hivyo kuna wakati huwa anashindwa pia kubaini madini na juzi kupitia kipindi "RapFix Live" rapper Kardinal Offishall aliweka wazi kosa alilolifanya

Nilimwambia kuhusu Drake mapema. Nilimwambia, Akon huyu dogo ni staa kwenye TV ni mkali balaa,” alisema Kardinall




Kardinal Offishall alikiona kipaji na uwezo wa Drake kabla ya YMCMB.


Kardinal, kama Drizzy, Anatokea Toronto, lakini alifanikiwa kutoka kabla ya Drake hajafahamika mwaka 2009 na mixtape yake So Far Gone
Nilikutana naye kabla hajaanza kufanya mixtape yake ya kwanza,” alisema. Kitu ambacho nakumbuka kuhusu Drake ni kama alikuwa na njaa ya kutoka kwenye uigizaji kwenda kwenye kurap



Baada ya kutoka nilienda na kumwambia Akon, “Nilikuambia”. Lakini hayo ni miongoni mwa mambo ambayo yamefanya kazi kwa Drake na YMCMB. Ana kambi nzuri

Unahisi Drake angekuwa hapo alipo kama Akon angemchukua

No comments:

Post a Comment